Karibu utangaze biashara yako hapa contact no 0758018458 AU Email:-mzimbilikiller@gmail.com



Breaking News

TAARIFA KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA HUAWEI GOOGLE YAZIPIGIA MARUFUKU.....!

GOOGLE KUPIGA MARUFUKU KAMPUNI YA HUAWEI KUTUMIA HUDUMA ZA ANDROID
GETTY IMAGES
Google imepiga marufuku kampuni ya simu ya pili kubwa duniani, Huawei, kutumia baadhi ya huduma kutoka mfumo wa uimarishaji kazi ya simu - Android, hatua ilio pigo kubwa kwa kampuni hiyo ya China.
Aina mpya za simu za Huawei hazitoweza kutumia baadhi ya programu tumishi kutoka Google apps.
Hatua hiyo inajiri baada ya serikali ya Marekani kuiorodhesha!
Google inasema "inafuata agizo hilo na kutathmini athari".

Huawei imesema itaendelea kutoa mfumo wa kuimarisha matumizi ya simu zake na huduma za baada ya mauzo kwa bidhaa zote za simu, tabiti ambazo tayari zimeuzwa au zile ambazo zingali zinasubiri kuuzwa kote duniani.
"Tutaendelea kujenga mfumo salama na wa kudumu, ili kutoa huduma nzuri kwa wateja wote duniani," imeendelea kuhakikisha.
GETTY IMAGES
Ina maana gani kwa wamiliki simu za Huawei?
Maswali mengi yameulizwa kuhusu athari ya mvutano huu kwa wateja wa bidhaa za Huawei barani Afrika.
Katika mitandao ya kijamii kwa mfano watu wamekuwa wakifuatilia mvutano na taarifa kuhusu Google kupiga marufuku Huawei kutumia huduma za Android na athari yake kwa simu za Huawei ambazo baadhi tayari wanazitumia:

2 comments: