Karibu utangaze biashara yako hapa contact no 0758018458 AU Email:-mzimbilikiller@gmail.com



Breaking News

JINSI MIILI YA WANADAMU INAVYOSHAMILI KICHOMWA KULIKO KUZIKWA1

Tanuru la mafuta ya dizeli la kuchoma wafu
Kuuchoma mwili wa binadamu baada kifo limekuwa ni jambo la kawaida kwa miaka mwingi miongoni mwa jamii za India na Nepal ambapo mchakato huu umekua ukifanyika mahala palipo wazi na utamaduni wa tangu enzi za kale . Kuanzia karne ya 19 , uchomaji wa maiti ulianza kutekelezwa katika maeneo mengine ya dunia .
Hata hivyo katika nyakati hizi , mchakato wa kuchoma maiti umekuwa ukifanyika kwenye matanuru au mahala pa faragha palipofungwa palipotengwa maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu idadi ya wa maeneo ya Afrika mashariki ambao wamechaguwa kuchomwa kwa miili yao kama njia ya kuihifadhi miili yao baada ya kifo badala ya njia ya kawaida ya kuzikwa kaburini.
Katika miezi ya hivi karibuni, kumeibua hisia tofauti katika eneo la Afrika Mashariki hususan nchini Kenya kuhusu kuchomwa kwa maiti baada ya mtu kufariki.
Wale wanaounga mkono uteketezwaji wa maiti wanasema mfumo huo wa mazishi ni wa kisasa na unapunguza gharama ikilinganishwa na maiti inapozikwa.
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mwanamazingira wa Kenya Profesa Wangari Maathai alichakua kuhifadhi mwili wake kwa kuuteketeza kwa moto
Image captionMshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mwanamazingira wa Kenya Profesa Wangari Maathai alichakua kuhifadhi mwili wake kwa kuuteketeza kwa moto
Kwa upande mwingine, wanaopinga wanadai kwamba utamaduni wa kuteketeza maiti ni wa kigeni unaoenda kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
Chimbuko la mjadala huu ni kuteketezwa kwa miili ya watu mashuhuri ; aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, Robert "Bob" Collymore, na mbunge wa upinzani Ken Okoth.
Wakenya wengine mashuhuri ambao miili yao ilitekekezwa kwa moto ni aliyekuwa mshindi wa tuzo ya Nobel na mwana mazingira Profesa Wangari Mathaialiyefariki mwaka wa 2011 na aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Kenneth Matiba.
Mwili wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini Kenya pia ulichomwa mwaka wa 2005.
Mwili wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, Robert "Bob" Collymore hivi karibuni pia ulichomwa
Image captionMwili wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, Robert "Bob" Collymore hivi karibuni pia ulichomwa
Kuna aina mbili za kuuchoma mwili wa binadamu, kulingana na Bwana Patel, afisa katika kituo cha kuchoma miili cha kariokor mjini Nairobi Kenya. ''Mwili ukifika hapa kwenye kituo chetu ndugu huchagua ni vipi mwili utachomwa, tuko na mashine na tuna kuni mnachagua kulingana na utashi wenu'', ameiambia BBC Bwana Harish Patel.
Kuchoma mwili kwa njia ya mafuta ya dizeli:
Kulinganza na Bwana Patel kuna mashine maalum zinazoweza kulinganishwa na tanuru ambapo mwili huingizwa ndani na kuchomwa kwa muda wa saa tatu hadi utakapoteketea kabisa na kuwa jivu. ''Tunauingiza mwili ndani ya mashine na kuchomea mwili ukiwa ndani ya jeneza kama ulivyoletwa hatubadilishi kitu. Mtu mmoja wa familia huchaguliwa ili awashe umeme anawasha na kisha tunasubiri mpaka saa tatu ziishe ili mwili uwe umeungua kabisa''.
Tanuru la kuni la kuchoma maiti
Image captionTanuru la kuni la kuchoma maiti
Baada ya saa tatu mifupa ya marehemu huwa bado haijaungua ndani ya mashine hiyo na mifupa huondolewa kwenye mashine ya kuchoma mwili na kuwekwa kwenye mashine nyingine maalumu inayofanya kazi ya kusaga mifupa ya marehemu na kuifanya kuwa majivu, anasema Bwana Patel.
Mashine hii hutumiwa kuteketeza mifupa ya mwili wa maiti baada ya mwili kuchomwa na moto ndani ya tanuru na dizeli au kwa kuni
Image captionMashine hii hutumiwa kuteketeza mifupa ya mwili wa maiti baada ya mwili kuchomwa na moto ndani ya tanuru na dizeli au kwa kuni
Kuchoma mwili kwa njia ya kuni:
Katika mchakato wa uchomaji wa mwili wa binadamu kwa njia ya kuni, mwili huwekwa kwenye kifaa cha chuma kilichotengenezwa mithili ya kichanja cha kuanika vyombo kisha rundo la kuni hupangwa juu na chini ya mwili, na kisha mwili hupakwa mafuta ya siagi na ufuta ili kuwezesha joto la moto kuuteketeza mwili kwa haraka.
Mafuta ya samuli
Image captionMafuta ya samuli
Kulingana na Bwana Harish Patel gharama ya kuuchoma mwili wa binadamu iwe kwa njia ya dizeli au kuni ni dola 400 za kimarekani.
Kuni huwekwa juu na chini ya kichanja cha kumchomea maiti huku maiti akiwekwa kati katika ya kuni
Image captionKuni huwekwa juu na chini ya kichanja cha kumchomea maiti huku maiti akiwekwa kati katika ya kuni

No comments